<p>Site Logo</p>

AIDS Trust Fund

<p>Site Logo</p>

17/8/2019 11:34 AM | Admin


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng akizungumzia hali ya UKIMWI Duniani ambapo alibainisha kuwa takribani watu milioni 37 wameambukizwa virusi hivyo,na kuwataka wananchi kuendelea na kujikinga maambukizi mapya kwa kufata elimu inayotolewa na wataalam wa afya. Alisema hayo mara baada ya matembezi ya hisani ya  kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI wa kudhibiti UKIMWI (ATF), Jijini Dodoma Novemba 24,2018 yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.